➤Shetani hapo mwanzo hakuwa adui wa Mungu. Yeye aliumbwa na
Mungu kama walivyoumbwa Malaika wengine. Alifanywa kuwa mkuu na akapewa utukufu mwingi na Mungu.
Baadaye akawa na kiburi na tamaa ya ukubwa, akataka
kumpindua Mungu, yaani akataka kuchukua nafasi ya Mungu.
ISAYA 14:13-14 “12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe
nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe
uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni,
Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa
mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya
mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.”
Akashawishi malaika wengine theluthi ya malaika ambayo ni zaidi
ya 30% ya malaika wote. Hii inadhihirisha ni jinsi gani alivyokuwa na kibali au
nguvu kubwa ya ushawishi.
UFUNUO WA YOHANA 12:4
“4 Na mkia wake wakokota theluthi ya
nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya
yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.”
Hapo mwanzo alikuwa ni LUCIFER
maana yake “MWENYE KUTOA MWANGA KAMA
NYOTA YA ALFAJIRI” Lakini sasa anaitwa SHETANI
maana yake “Adui, Mpinzani, Mshindani,
Mleta vizuizi”.
Shetani alianzia upinzani kwa Mungu pale alipokataa kufuata
maongozi yake (Mungu) na kutaka yeye ndiye awe kiongozi.Maana yake akawa ni
muasi kama yalivyo majeshi ya waasi. Waasi hupigana na serikali iliyopo
madarakani hivyo na shetani naye alifanya vivyo hivyo.
UFUNUO 12:7-9 “7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na
malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na
malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9
Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani,
audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa
pamoja naye.”
Mikaeli alikuwa ni Jemedari Mkuu na ndiye aliyeongoza jeshi
la Malaika waliokuwa upande wa Mungu kupambana na Shetani na jeshi lake.
DANIELI 12:1 “1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari
mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu,
mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na
wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika
kitabu kile.”
Mikaeli huhusika katika mapambano makali dhidi ya shetani.
DANIELI 10:13,21 “13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi
alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao
wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa
Uajemi. 21 Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala
hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.”
Shetani alimdanganya Hawa ale matunda ya mti wa ujuzi wa
mema ya ubaya ili yeye(Shtani) apate faida ya kuwa na wafuasi wengi katika
chama chake.
Shetani huyo huyo huwapinga watoto wa Mungu kumtii Bwana
Yesu na badala yake wamtii yeye (shetani). Shetani hutuzuia kuomba, kusikiliza
neno la Mungu au kujifunza kwa njia ya mtandao kama hivi unavyojifunza, bila
shaka wewe mwenyewe sasa ni shahidi kwamba kulikuwa na kitu ndani kinakuzuia
kusoma ujumbe huu lakini Mungu kwa kuwa anatupenda ametuwezesha mimi na wewe
tujifunze ujumbe huu. Unapoona kuna upinzani wowote ili usiende kuhudhuria
ibada au semina za neno la Mungu kataa upinzani huo na mwambie Malaika Mikaeli
akuagizie kikosi kazi kije kushughulika na vizuizi hivyo. Pia unapotaka kusoma
biblia au kuomba ukiona kuna upinzani fanya hivyo hivyo na matokeo yake utaona
unamshinda shetani kwa sababu jeshi lililo upande wako ni kubwa kuliko lile
lililo upande wa Shetani.
Kataa kila namna za upinzani zinazoinuka ndani yako na
kukwambia kuwa unaweza kufanya lolote tu. Roho hizi za upinzani zimewaingia
watu na wao kuanza kumpinga Mungu kama alivyoanza Shetani. Namna yote ya kujikoboa ngozi mweusi kuwa mweupe na
mweupe kuwa mweusi hizo zote ni roho za upinzani. Kufanya hivi ni kumkosoa Mungu
kwamba alivyokuumba sivyo. Unategemea nini unapomwambia mwalimu wako kwamba
alivyokufundisha si sahihi bali wewe ndiye unajua vizuri halafu mwisho wa siku
unafanya mtihani wake na msahihishaji akiwa ni huyo huyo? Unadhani ni
ninikitakachotokea?
WARUMI 9:20-21 “20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani
umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani
kuniumba hivi? 21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la
udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?”
Neno la Mungu katika 1 WAKORINTHO 11:10 linamtaka mwanamke
anaposali au anapohubiri afunike kichwa, namna yote ya kuwa kinyume na neno
hili ni roho za upinzani.
Kubadili matumizi ya
haja kubwa kuwa sehemu za kufanyia tendo
la ndoa zote hizi ni roho za upinzani zinazopingana na uumbaji wa Mungu.Nafahamu wengine wanafanya mambo hayo kwa
shinikizo la mtu Fulani lakini ni vyema ikafahamika kwamba wale malaika walio
shawishiwa na Shetani wanakula sahani moja au wanapata adhabu moja na shetani. Hivyo
kama na sisi tunafanya mambo kwa sababu Fulani anataka basi tujue kwamba
kikombe atakacho kinywea ndicho tutakacho kinywea wala hakuna sababu yoyote ya
kujitetea. Adam na Hawa walijitetea lakini uttetezi wao haukusaidia kwa lolote.
WARUMI 1:25-27, 32
“25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu
kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa
milele. Amina. 26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata
wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi
ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata
nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Ambao wakijua sana hukumu
ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo,
wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.”
Tusipende kufanya mambo eti kwa sababu karibu jamii yote
inayotuzunguka inafanya hivyo. Fahamu kwamba kila mmoja atalichukua furushi
lake mwenyewe (WAGALATIA 6:5).
Kwa jitihada zako huwezi lakini Ukimuomba Mungu yeye ni
mwenye rehema, atakusaidia.
Je, unataka kuokoka ili uwe na uwezo wa kuzishinda roho za
upinzani?
Bonyeza hapa===è NAHITAJI MSAMAHAWA DHAMBI
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: