» » SOMO: OMBENI WALA MSIKATE TAMAA


Na Ev. Zachary John Bequeker
+255-625-966-236
+255-758-590-489
LUKA 18:1 "Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa."

Kukata tamaa ni ishara ya kukosa imani. Kukosa imani hakumfurahishi Mungu wetu WAEBRANIA 11:6 "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao."

Tusikate tamaa wala kulalamika na kunung'unika bali tuendelee kuomba. Manung'uniko yanaweza kutufanya tupigwe na shetani. 1 WAKORINTHO 10:10 "Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu."

MIFANO YA WATU WALIOOMBA BILA KUKATA TAMAA

1. YAKOBO
Yakobo aling'ang'ania kubarikiwa (MWANZO 32:24-29)

2. HANA
Mwanamke Hana aliomba kwa bidii ili apate mtoto (1 SAMWELI 1:10-18,20)

3: DANIELI 
Danieli aliomba bila kukata tamaa (DANIELI 9:17-22).

4. DAUDI
Daudi alimuomba Mungu wakati wote hakuchoka. ZABURI 55:16-17 "Nami nitamwita Mungu, Na Bwana ataniokoa;Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu."

Wewe nawe omba bila kukoma.

Ungana na group la INJILI HALISI MINISTRY la Facebook kwa kubonyeza hapa===> INJILI HALISI FACEBOOK

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply