» » SOMO: BIDII ILEILE

Askofu David Chamotto na Katibu Mkuu wa kanisa la FGBF Tanzania, Askofu Nathan Meshack.

»Baada ya kujifunza mapenzi ya Mungu ni vyema tukiyatenda. Mtu anayeyajua mapenzia ya Mungu halafu hayatendi anafananishwa na nguruwe aliyeoshwa kisha akarudia uchafu wake, pia anafananishwa na mbwa aliyeyarudia matapishi yake; na mtu huyo atapigwa sana(LUKA 12:47).

»Ili kuweza kuyatendea kazi yale uliyojifunza ni lazima kuwa na bidii wala Si suala la neema pekee. 

»Ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu.

»Neema hufanya kazi kwa mtu anaye/aliyechukua hatua kutenda. Kama unahitaji neema ya kuomba ni lazima uanze kuomba kisha neema itakufunika.

»Thawabu ya Mungu huwa kwa watu wanao dhihirisha bidii ileile bila kuchoka.

»Ni lazima kujipima moto wako/bidii yako kuwa ni ileile au imepungua. Kama ulikuwa mwombaji, je unaomba kwa bidii ileile uliyokuwa nayo au umeshachoka? Kama Ulikuwa mtoaji, unatoa kwa bidii ileile au umeshalegea? Kama Ulikuwa unahubiri, je unahubiri kwa bidii ileile au umeshachoka?, kama Ulikuwa unasimama katika viwango vya usafi na utakatifu, unaendelea au umeshaghairi? 

WAEBRANIA 6:9-12 ".....kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu hata mwisho; ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu".

»Tunapaswa kuidhihirisha bidii ile ile bila kulegea, uvivu wowote hauhitajiki kuwepo kwa mtu wa Mungu. 

»Wavivu hawaingii mbinguni kwa maana wao ni goigoi na wanyonge .

»Mtu mvivu anafananishwa na bawaba(MITHALI 26:14). Bawaba inapochoka baada ya kuwepo kwa mlango kwa muda mrefu huanza kuwa inalia, kila unapofungua mlango unasikia " viiiiiiiiii, gogogogogo" ili isipige kelele inatakuwa kuiwekea grisi au oil.

»Mitume na Manabii wanapata ulaji kwa sababu ya watu kuwa wavivu; kila kitu wanataka wafanyiwe. Watu hawataki kuomba ila wanataka shortcuts za maji ya upako, mafuta ya upako, sabuni za upako, vitambaa vya upako, mchanga wa upako n.k. Biblià inaposema "kuwapaka mafuta" ni mafuta ya Roho Mtakatifu(YAKOBO 5:14). Acha uvivu, soma Neno la Mungu uelewe linasemaje.

» Biblià inasema katika MITHALI 28:19 kuwa mtu aliye mvivu hupata umasikini wa kumtosha, na mtu ambaye ni maskini wa kiroho hana Neno la Mungu, hana Maombi na mtu huyu hawezi kuingia mbinguni.

»Ukiwa mvivu utapata utapia mlo wa kiroho. Tunapolisikiliza Neno la Mungu na kuomba tunapata lishe bora ya Kiroho.

»Baada ya kuokoka(kuzaliwa mara ya pili) ni lazima tuhakikishe tunahudhuria kiliniki ya kiroho kama siku zetu  zilivyopangwa(siku zote za ibada na tukiwa nyumbani pia).

»Mtu anapookoka anakuwa na moto(bidii) lakini kadri siku zinavyoenda huanza kulegea. Haipaswi kuwa hivyo kwetu katika Jina la Yesu.

»Tia bidii ile ile ya mwanzo ili tumfanye Mungu ajivunie sisi, ajionee fahari katikati yetu kama alivyojionea fahari kwa AYUBU. Ayubu pamoja na majaribu alibaki na bidii ileile na msimamo ule ule bila kubanaika(AYUBU 1:6-8,21-22, AYUBU 2:1-8).

»Tuwe kama askari vitani. Askari haogopeshwi na maiti, mwenziye akipigwa yeye hupita mbele na kuendeleza mashambulizi.

»Kama ni kuomba, kuhubiri, kushuhudia, kuongozawengine, kutoa ni lazima kuwa na bidii ile ile.

»Shetani hulenga vitu vyetu na afya zetu ili tulegee na tumkufuru Mungu. Tusilegee bali tuendelee na bidii ile ile.

»Mungu ndiye atiaye bidii ileile na inapaswa bidii yetu iongezeka(2 WAKORINTHO 8:16-22).

»Tuidhihirishe bidii ile ile tukiyatenda mapenzi ya Mungu nasi tutashinda (1 YOHANA 2:12-17).

»Kizuizi kikubwa cha kutenda kazi ya Mungu ni UOGA. Mungu hakutupa roho ya woga(2 TIMOTHEO 1:7, 1 YOHANA 4:18) Ili tuidhihirishe bidii ile ile ni lazima kuwa mbali na woga; kama unapenda kupendwa na kila mtu huwezi kuyatenda mapenzi ya Mungu.

»Mwombe Mungu akuwezeshe kuwa na bidii ile ile, kama Ulikuwa umelegea mwambie Mungu akutie nguvu tena.

Preached by Askofu Nathan Meshack.

Written by Zachary John Bequeker , Mwanza- Tanzania +255-625-966-236 Zacharybequeker@gmail.com

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply