Na Mwinjilisti Zachary John Bequeker
Hapa tutaangazia mambo kumi kama ifuatavyo.
1. Pesa
=> watu huwa wakitumia muda mwingi wakitafuta pesa kuliko kuutafuta USO wa Mungu, kwa kuomba na kusoma biblia.
√Mathayo 6:19-34
=>Sina maana ya kwamba uache kazi au uache kutafuta pesa, Bali tumfanye Mungu kuwa wa muhimu kuliko pesa.
2. Vyombo vya habari
=> Internet, Magaeti,Tv, simu n.k tunapaswa tutumie kwa kiasi.
3. Kanisa/Dini
=>Watu wengi huamini Dini kuliko kumwamini Yesu kristo aliye njia, kweli na uzima.Nenda kanisani na uishi kwa kulifuata neno la Mungu na so mapokeo ya kanisa au Dini.
4. Mahusiano
=> Mahusiano yetu kati ya wazazi,ndugu,jamaa,wafadhili wetu, watoto,wafanyakazi wenzetu,wakuu wetu wa kazi, boyfriends/girlfriends ......hawa wote wanauwezo mkubwa wa kututenga au kupoza upendo wetu kati yetu na Mungu. Ni asili yetu wanadamu kuwa na Mahusiano, lakini tusiruhusu moja ya uhusiano huu kuwa kuwa na nguvu kuliko Mungu .
KUMBUKA: Mungu ametuagiza tupendane 1 Yohana 3:11….Kwa hiyo tunapopendana,tunatimiza agizo la Mungu. Lazima tuhakikishe kwamba tunampa Mungu muda wa kutosha(ample time) kila siku.
Uhusiano wa girlfriends, boyfriends na wakuu wetu wa kazi ni uhusiano hatari sana ambao una 100% za kutuweka mbali na Mungu wetu. Tuwe makini na wakuu wetu wa kazi na tusiwe na girlfriends au boyfriends kwani ni dhambi.
Waefeso 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”
5. Ratiba(Routine)
=> Hakikisha unatenga muda wa kuwa na Mungu wetu.
Katika ratiba zetu lazima kuwepo na muda wa Kusoma neno na kuomba. Na mruhusu Mungu akuongoze.
6. Kazi zetu
=>Kazi zetu hutufanya kuwa mbali na Mungu. Kwa maana watu wengi huwa tunatumia muda mwingi kwa kazi na kumsahau Mungu. Wakati mwingine tunajikuta katika wakati mugumu tunapokuwa kazini. Tufanye kazi kwa bidii na tutenge muda wa kuwa na Mungu wetu pia.Tusiwe kama Martha Bali tuwe kama Mariam Luka 10:38-42
7. Our hobbies
=> Our hobbies can consume a lot of time. Hobbies zetu hutuchukulia muda mwingi sana.
8. Kuhitaji baraka za Mungu kuliko Mungu mwenyewe
=> Tuutafute kwanza ufalme wa Mungu Mathayo 6:33
9. Wachungaji wetu
=> Wachungaji nao wanaweza kututenga na Mungu. Wachungaji wengi huaminisha waumini kuwa wao Ndio wanajua kila kitu…….na sababu hiyo husema hakuna haja ya kuhangaika kusoma Vitabu vya neno la Mungu tukiwa nyumbani. Hebu fikiri kwa MTU anayeenda kanisani mara moja kwa juma maana yake anailisha roho yake mara moja tu kwa siku saba. Je,! Unaweza kuishi juma uzima kwa kula mlo mmoja tu kwa siku zote hizo?
KUMBUKA: Si wajibu wa wachungaji kutulisha kila tunachohitaji Kiroho Bali ni Wajibu wetu kulitafuta neno la Mungu wakati wote.
10. Sisi wenyewe
=> Kwa asili tu wenye dhambi na tunapofuata asili yetu tuna kuwa mbali na Mungu.
Kwa sababu hiyo nasi ni vyema tukaishi kwa kumfuata Mungu wala tusifuatishe matakwa ya miili yetu.(tamaa zetu wenyewe). Tujikane na tuishi ndani ya Kristo Warumi 7:15-21
Tumruhusu Mungu aichunguze na kuitengeneza mioyo yetu. Zaburi 139:23-24.
Ni Mimi Ev Zachary John Bequeker - Mwanza
Wasiliana nami:
Barua pepe: zacharybequeker@gmail.com
WhatsApp/IMO/Telegram/Direct call/SMS +255625966236
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
Ni ruksa ku-comment.
ReplyDelete