Mkewe Lutu baaada ya kuikumbuka Sodoma na kugeuka nyuma.
WAFILIPI 3:12-13 "Si
kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo
ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na kristo Yesu.
Sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma,
nikiyachuchumilia yaliyo mbele” .
Mpendwa katika Bwana
Yesu Kristo karibu tujifunze pamoja neno hili lililo la msingi katika
maisha yetu ya kila siku.
Ni mimi Ev. Zachary
John Bequeker – Mwanza Tanzania +255 625 966 236 / +255 758 590 489. Email:
zacharybequeker@gmail.com
ð
Tusiwe watu wa kujisifia mambo mazuri
tuliyofanya huko nyuma. Sisemi kwamba kujisifia mambo mazuri tuliyoyafanya huko
nyuma ni vibaya; la! Jambo kuu la msingi ni kujihoji kwamba “je, nilivyo sasa
ni sawa na nilivyokuwa zamani?” Ukiona kuna tofauti, jibu limekuwa sasa
nimebadilika(nimelegea) basi hakuna haja ya kujisifia.
ð
Kama tulikuwa waombaji,wahubiri, watoaji, wenye
bidii katika kutenda mema na sasa tumeacha hayo, Basi hakuna haja ya kujisifia.
ð
Tusiangalie jinsi tulivyoanza bali tuangalie
namna gani tutakavyomalizia kwani Mungu huangalia umaliziaji na si uanzaji.
ð
Kama tulianza vizuri na kumaliza vibaya sisi
hatutakuwa wa thamani mbele za Mungu EZEKIELI
18:24 “Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake na kutenda uovu, na
kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu …….katika matendo yake yote
ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo……”
ð
Maisha ya wokovu ni maisha ya mashindano kama RIADHA. Katika RIADHA Mshindi
hapatikani mwanzono bali mwishoni.
ð
Mkewe Lutu aliokolewa kutoka Sodoma, akiwa
njiani aliikumbuka Sodoma tena mara
akageuka nyuma akawa nguzo ya chumvi. Mkewe Lutu alianza vizuri ila umaliziaji
ulikuwa mbovu kwani aliyakumbika yaliyonyuma(Sodoma) . Hivyo TUSIWE KAMA MKEWE LUTU LUKA 17:32.
ð
Sauli kabla ya kuokoka na kuwa Paulo, kazi yake
ilikuwa ni kulitesa kanisa la Mungu na alipata ujira kwa kazi hiyo. Lakini
baada ya kuokoka alipokutana na magumu, mazito na majaribu hakutaka kuyakumbuka
maisha yake ya raha kabla ya kuokoka. WAFILIPI
3:7-8.
TUNAPOYATAFAKARI YALE YALIYOPITA,
HUTUPUNGUZIA KASI YA KUENDELEA MBELE. Kuyakumbuka yaliyopita kunasababisha
kupungua kwa nguvu ya Mungu ndani yetu, Kwani tunapokumbuka mabaya
tuliyotendewa hatutaweza kusamehe na kutenda meme kwa wengine bali tutabakia na
kinyongo ndani yetu. Na kinyongo ni dhambi.
Ev. Zachary John
Bequeker – Mwanza Tanzania +255 625 966 236 / +255 758 590 489.
Email: zacharybequeker@gmail.com
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: