» » SOMO: DHAMBI NI NINI?




»Dhambi ni uasi (1 YOHANA 3:4).
»Neno "dhambi" linatokana na neno la Kiyunani "HARMATIA" ambalo maana yake katika Kiingereza ni "MISSING THE MARK", kwa Kiswahili tungesema ”KUIACHA ALAMA" au "KUUACHA MSTARI".
Alama hii au mstari huu ni Neno la Mungu(ZABURI 119:9).

»Dhambi ni zaidi ya kuua, , kusema uongo, kuzini au kufanya uasherati, kuiba, kutotii wazazi(MATHAYO 19:18-19).

»Masengenyo, hasira(MATHAYO 5:21), matusi, uvutaji wa sigara , bangi, ulevi wa sigara au madawa ya kulevya, rushwa, ushirikina, ibada ya sanamu na mambo mengi yanayofanana na haya, yote ni dhambi.

»Dhambi ni zaidi ya hizo zilizoorodheshwa hapo juu👆, bali ni namna yoyote ya kukengeuka kwenda kushoto au kulia na kuacha kufanya yale tuliyoamriwa na Mungu katika neno lake(KUMBUKUMBU LA TORATI 5:32, YOSHUA 1:7).

»Neno la Mungu limetuagiza kuomba, kama huombi tayari ni dhambi.                  (1 THESALONIKE 5:17, 1 SAMWELI 12:23).

»Tukiliasi neno la Mungu na kufanya tunayoyataka wenyewe Kama Adamu na Hawa walivyokula matunda waliyokatazwa, kinyume na Neno la Mungu; kufanya hivyo ni dhambi.

»Hatupaswi kucheza na dhambi na kuona kama " starehe" na raha za dunia.

»Dhambi ni machukizo makubwa mbele za Mungu kiasi kwamba tufanyapo dhambi, maovu hayo yanatufarikisha au kututenganisha na Mungu mara moja. Dhambi hujenga ukuta kati yetu na Mungu, kwa sababu hiyo Mungu hataki kutuona au kutusikia tunasema nini! (ISAYA 59:1-2). Mara Adamu na Hawa walipofanya dhambi , Mungu hakutaka kuwaona tena hivyo akawafukuza katika bustani ya Edeni na kuweka Makerubi na upanga wa moto uliogeuka huko na huko kuilinda njia ya kuingilia bustanini (MWANZO 3:24).

»Kumbe hata nasi tunapofanya dhambi, Mungu hutuondoa katika ufalme wake na huondoa ulinzi wake kwetu, hivyo shetani kuwa na nafasi ya kutawala maisha yetu.

»Msahara wa dhambi ni mauti (WARUMI 6:23) na wote watendayo dhambi hawataingia mbinguni bali moto wa milele( UFUNUO 21:8).

»Saa ya wokovu ni sasa( 2 WAKORINTHO 6:2).

OKOKA SASA MUDA NDIO HUU USISEME KESHO, KESHO SIYO YAKO, YAKO ILIKUWA NI JANA NA LEO YA MUDA HUU ULIO NAO TU.

NI MIMI EV. ZACHARY JOHN BEQUEKER - MWANZA +255625966236

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply