» » SOMO: KUKUSANYA PAMOJA NA YESU

Askofu David Chammoto- FGBF Mwanza(juu), Askofu Jacob Magesa- FGBF JIMBO LA KAGERA( Chini), Katibu Mkuu wa FGBF Tanzania - Askofu Nathan Meshack, FGBF IRINGA

»Katika mpango wa Mungu kila mtu anatakiwa kufanya kazi, Kama mtu hafanyi kazi hatakiwi kula (2 WATHESALONIKE 2:10). Kazi ni ya muhimu sana kwa kila mtu kwani huwezi kula kama hufanyi kazi hivyo ni lazima tufanye kazi. 

»Tunapofanya kazi lazima tutaona faida ya ile kazi (2 TIMOTHEO 2:6) Kila mtenda kazi anastahili posho lake (MATHAYO 10:10b). Mtu yeyote ambaye hatendi kazi hawezi kupata posho. 

»Mungu hutubariki kupitia kazi za mikono yetu (KUMBUKUMBU LA TORATI 18:18).

»Mungu baada ya kuumba kila kitu hakumuacha Adamu akae tu pasipo kufanya kazi, bali alimuagiza ailime bustani. Si kwamba hakukuwa na Chakula, la hasha! Katika bustani ile kulikuwa na mazao ya kila aina ambayo Adamu hata asingefanya kazi maisha yake yote asingekosa Chakula. Mungu aliona kama Adamu angekuwa anakula tu angedhoofika ndipo akamuagiza ailime bustani ili ale iliyo halali yake na pia mwili usidhoofike ( MWANZO 2:15-17).

»Mtu hawezi kuishi bila kazi.


»Kama hufanyi kazi ya Mungu ni lazima utafanya kazi ya Shetani. Kazi za Shetani ni masengenyo, kudhurura, uongo(ubuyu) n.k.

»Unapokuwa busy na kazi ya Mungu si rahisi kuingia katika mitego ya shetani.

»Adamu alikuwa busy ndipo Shetani akaona amwendee mkewe, Hawa. Hawa alidanganyika kwa sababu alikuwepo tu bila kazi, matokeo yake akaanza umbeya na nyoka na hatimaye akadanganyika.

»Tunapaswa tuwe tayari kwa kila kazi njema (TITO 3:1).

»Kama jinsi tulivyo na kazi zetu za mwilini, Mungu pia ametuchukua ili tufanye kazi katika shamba lake (MATHAYO 20:1-16) Mungu hapendi kuona watu wasio na kazi.

»Mshahara unategemeana na kazi uliyopewa na bidii yako, haijalishi umeanza mapema kiasi gani bali ni kiasi gani cha kazi umefanya. Kama umefanya kazi kwa ulegevu pamoja na kuanza alfajiri, saa tatu, saa Sita au saa tisa(Mapema) mwingine akaanza saa 11 jioni na akafanya kazi kwa bidii atakuwa amefanya kazi kubwa sawa au zaidi ya aliyeanza alfajiri hivyo atapata mshahara mnono.

»Bidii yako ndiyo mshahara wako. Haijalishi umeokoka siku nyingi kuna watu wanaweza kuokoka au waliokoka hivi karibuni na wakatenda kazi kwa bidii hivyo wanakuwa na ujira mkubwa siku ile .

»Watu wanaojiita wamekomaa kiroho ni wasumbufu na wagumu kiasi kwamba hawapindiki, chochote wanachoambiwa kuhusiana na kazi ya Mungu wao kusema " hilo mimi nalijua, wewe ndio umelisikia leo?" " Nasikia mnaambizana, tuombe jamani tusiache kuomba; hivi mnadhani siku hizi mnaomba ? Sisi zamani tulikuwa tukiomba haswaa".

» Mwenye shamba aliwapa dinari wote kwa sababu wale wa Asubuhi hawakufanya kazi kwa bidii walitaka kubakiza kiporo ili na siku ya pili waifanye kazi hiyo wapate mshahara tena, Mwenye shamba hakutaka kazi yake ilale, alitaka imalizike siku hiyo hiyo tu, ndipo akaamua kuongeza wafanyakazi wengine ili kazi yake imalizike haraka na kwa kuthibitisha hilo tunaona wale wengine waliajiriwa ukiwa umesalia muda kidogo tu. 

»Sisi ni wafanyakazi pamoja na Mungu (1 WAKORINTHO 3:9).

»Tunapaswa kukusanya pamoja na Bwana(LUKA 11:25) .

»Unapokusanya na Yesu, yeye(Yesu) anakuwa upande wako na anakutumia kwa namna ya kushangaza. Unapokusanya na Yesu, Mungu lazima alithibitishe Neno lake kwa ishara na miujiza, katika hali hii jambo la kuliepuka ni kiburi; Unapotumiwa na Mungu kwa viwango vya juu usiinuke na kukuona wewe ni wewe kwani matokeo yake ni uasi. Tunapofanya tujue tumefanya yaliyotupasa kufanya (LUKA 17:10).

»Tuifanye kazi ya Mungu kwa furaha.

»Ukiwa huna uwezo wa kushinda dhambi huwezi kukusanya pamoja na Yesu(kuhubiri wengine).
OKOKOKA SASA, 

Written by Zachary John Bequeker FGBF CHURCH MWANZA +255-625-966-236

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply