»Kinyongo ni hasira za ndanindani, tabia za kutopenda watu wengine.
1:DHAMBI YA KINYONGO
»KINYONGO ni dhambi iwazingayo watu wengi. Hii ni moja ya dhambi za moyoni. Mtu mwenye KINYONGO moyoni mwake huumbika mawazo ya kinyongo na mtu au watu wengine kutokana na mafanikio au kuinuliwa kwao. Ndani ya mtu huyo(mwenye kinyongo) huwa na mawazo ya "UMIMI".Mtu huyo hujiuliza na kufikiri hivi" Kwa nini Fulani ana kitu Fulani au kwa nini mtu amefanya hivi au vile na si mimi? Ana mafanikio yale na yale na si mimi? ".
»Mtu anaweza kucheka nje lakini ndani kuna vita vikali kwa sababu ya kinyongo(YAKOBO 4:1; WARUMI 7:23, 15-19).
»Mungu pekee ndiye anayejua ndani ya moyo wa mtu kuna nini (1 SAMWELI 6:7; MATHAYO 12:32-35).
2:MADHARA YA KUWA NA KINYONGO
» Dhambi ya KINYONGO INA madhara makubwa kwa mtu anayeifuga.
» Dhambi hii iko ndani ya moyo wa mtu, haionekani kwa nje bali matunda yake huidhihirisha(MATHAYO 12:33).
»Moyoni mwa KAINI kulikuwa kumejaa KINYONGO. Kwa nje alionekana mwenye upendo kwa ndugu yake HABILI. KAINI alipomwambia Habili twende uwandani, Habili hakusita kwa sababu alijua ameambiwa kwa wema tu kumbe KAINI alikuwa na lengo la kumuua nduguye(MWANZO 4:8). Mungu aliuona moyo wa Kaini mapema akamwonya lakini hakutaka kusikia/kutii (MWANZO 4:6-7). Baada ya kifo cha Habili Mungu alimlaani Kaini (MWANZO 4:9-13).
»Dhambi ya KINYONGO imefanana na HEWA KATIKA PUTO. Kadri hewa inavyozidi kuongezeka ndani ya Puto mduara wa Puto huzidi kuongezeka na mwisho wake PUTO HUPASHUKA. Puto likishapasuka hutupwa pasipo kushonwa au kutiwa kiraka. Ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye KINYONGO. Kinyongo huongezeka tena na tena na mwisho huleta madhara yasiyoweza kurekebika kama kaini alivyosema dhambi yake haichukuliki na hawezi kurekebisha kwa kuwa tayari Habili amekwisha kufa! (MWANZO 4:13).
»Kumbe kinyongo huweza kusababisha kuua pia humsababishia mtu mwenye kinyongo kupatwa na magonjwa kama vile madonda ya tumbo, presha, kisukari na mengineyo mengi kwa sababu mtu unapokuwa amejaza chuki mwilini mwake, moyo hubadili mienendo/utendaji kazi wake na kutenda jinsi isivyo sahihi. Hebu relax kwa nini ufe mapema ndugu yangu?
»Mtu mwenye kinyongo pia ni mtu mwenye roho ya kisasi.
»Bwana ametuagiza tusiwe wala tusifuge kinyongo ndani ya moyo yetu(MAMBO YA WALAWI 19:18)
»Kinyongo huleta UADUI.
»Tunapaswa kutii amri ya pili ya UPENDO, tuwapende jirani zetu (watu wote) na kuwaombea mema (MATHAYO 5:43-44, 19:19, 22:39 ; LUKA 10:27, WARUMI 13:9 ; YAKOBO 2:8)
» Tusiwe watu wa kulipiza visasi, kisasi ni cha BWANA (WARUMI 12:17-21).
3: JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KINYONGO
»Hii ni dhambi ikaayo ndani ya moyo wa mtu (WARUMI 7:20).
»Dhambi hii unaweza Kutoka tu tunapoichukia, kuijutia na kutubu baada ya kujua madhara yake.
»Ni OLE kwa Mkristo ambaye pamoja na kuokolewa bado ana kinyongo maana atapatwa na mauti ya pili(WARUMI 7:24).
»Tunapogundua kuwa tunadhambi ya kinyongo ndani mwetu, tutubu kwa machozi na kumwambia Bwana aitahiri mioyo yetu. Tukiomba kwa bidii Mungu ni mwaminifu ataiondoa na KUTUTAKASA. Tukitakaswa tutawapenda hata watu wanaotuudhi . Tena tutawaombea mema siku zote, iwe ndugu zetu, jirani zetu, wake/waume zetu, watoto wetu, wanafunzi wenzetu na wafanyakazi wenzetu.
»Yesu alimpenda ADUI yake akamwita RAFIKI(MATHAYO 26:47-50).
» Stefano alipokuwa anapigwa kwa mawe, damu inachuruzika, aliwaombea mema watu waliokuwa wakimtupia mawe afe kwa sababu ndani yake hakukuwa na Kinyongo ( MATENDO YA MITUME 7:58-60).
»Mungu atatuondolea dhambi ya kinyongo tunapotubu ikiwa Kutoka moyoni mwetu tumemaanisha kuwasamehe watu wote waliotukosea (MATHAYO 6:14-15).
†Mshahara wa dhambi ni kutupwa katika moto🔥 wa milele(WARUMI 6:23) Kinyongo ni dhambi, bila kutubu moja kwa moja ukifa ni motoni.
Bwana ampe kila mmoja ROHO WA NEEMA NA KUOMBA hadi atakaswe katika Jina la Yesu!
Kama wewe hujaokoka, unahitaji kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako ili uiepuke adhabu ya moto wasiliana nami kwa +255 625966236/+255 758590489.
Ni mimi Ev. Zachary John Bequeker- Mwanza Tanzania.
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: