MHUBIRI: ASKOFU NATHAN MESHACK
MAHALI: FGBF MWANZA 28.01.2018
MWANDISHI: Zachary John Bequeker
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Katibu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Askofu Nathan Meshack
» Majumbani mwetu kuna vyombo vya kila aina. Kila vyombo hutengwa kutokana na kazi zake. Kuna vyombo vya gharama na kawaida. Vyombo vya thamani huwekwa kabatini, na huchukua muda mrefu bila kutumika wala kuoshwa.
Vyombo vya kawaida, visivyo vya thamani hutumika mara kwa mara; kwa sababu hiyo, huhitajika kuoshwa mara kwa mara. Mara nyingi, vyombo vya gharama hutumika maalum kwa ajili ya wageni ambapo vyombo vya kawaida hutumiwa na watoto kwa sababu vyenyewe havivunjiki(bondo).
Tatizo hutokea pale unaposafiri na watoto kwenda ugenini. Watoto wakipewa vikombe vya udongo hukataa kwa sababu walishazuiwa na wazazi wao kuvitumia na pia hawajavizoea.
Kumbe ni vyema hata watoto tukawapa ruhusa ya kuvitumia vyombo vya thamani kama uma(fork), vijiko(spoons), vyombo vya udongo na pia tuwazoeshe kulia mezani, siyo siku unaenda hotelini, watoto wote wanakataa kulia mezani.
Hakuna cha kusema vyombo hivi ni vya wageni, ni lazima vitumike hata kwa watoto na tuwafundishe namna ya kuvitumia ili tukienda nao ugenini au hotelini wasitutie aibu. Bondo(plastic) zingine huwa Si nzuri kuzitumia.
Mfano kuna sahani au vikombe vya bondo unapokuwa unaviosha vinatoa nyuzinyuzi na vingine hukwanguka. Hivyo kwa kulinda afya za watoto wetu ni vyema wakatumia vyombo vya mifupa, udongo na kama ni (bondo)plastic ziwe zisizo toa nyuzinyuzi wala kukwanguka ili kuwakinga watoto wetu na magonjwa kama ya kansa.
Vyombo vya wageni havitumiki wala havisafishwi sana. Vyombo vinavyotumika mara kwa mara huoshwa mara kwa mara.
Kama unazingatia Milo mitatu kwa siku, maana yake vyombo hivyo vitaweza kuoshwa mara tatu kwa siku. Hata katika Kanisa ni vivyo hivyo (YOHANA 15:1-2). Katika nyumba ya Mungu, kanisa(watu) ni vyombo vinavyofanya kazi ya Mungu.
Vyombo vinavyofanya kazi ya Mungu sana na Mungu huvisafisha sana. Ukiwa wa kabatini(kukaa bila kutumika) huoshwi bali wa jikoni(anayefanya kazi ya Mungu) huoshwa wakati wote. Tatizo la vyombo vya kabatini, hata watoto au wajakazi(house girls) wanapovivunja huvirudisha pale pale na wala hutagundua kuwa vimevunjika na ni nani aliyevunja.
Siku ukigundua ukiwauliza hata wao watakuruka na utaona wanashangaa " kwani nini mama?" " Si ulitukataza tusivitumie, sisi hata hatujui!" . Mbaya zaidi ni kwamba umeacha ukisema vya wageni lakini ukiondoka watoto na wajakazi huvitumia.
Hata katika kanisa kuna watu wanaweza kupatwa na matatizo kama kuugua, kufiwa na mengineyo na wala wengine wasijue kwa sababu wao hawako tayari kutumika katika nyumba ya Mungu.
Unapokuwa unatumika kanisani watu watakutambua hivyo hata ikitokea siku moja tu haupo kila mmoja atauliza Fulani yuko wapi mbona simuoni Leo?. Huwezi kutambulika kama wewe hutumiki.
Ni vyema kujulikana kwa Mungu na kanisani pia. Katika nyumba ya Mungu kuna watu wenye karama tofauti tofauti na Mungu humtumia kila.mmoja kwa nafasi yake aliyonayo.Tunapotumika Mungu hutusafisha sana ili tuzidi kutumika na tuwe vyombo vinavyomfaa Bwana kwa kazi njema (2 TIMOTHEO 2:20-21) Tuwe vyombo vya kumfaa Bwana ili tuzidi kusafishwa sana.
Tunapotumika, tunasafishwa na tunakuwa safi na nguvu za giza hazitatuweza kamwe kwa sababu Shetani hawezi kuweka makao kwetu.
Vyombo vinavyotumika (Chombo cha Bwana) huwa na misukosuko mingi lakini hakiachi kufanya kazi. Watu wanaotumika huudhiwa (MATHAYO 5:10), Paulo Mtume aliudhiwa kwa sababu alikuwa akihubiri injili, hivyo na sisi tsione ajabu kuudhiwa kwa sababu ya kumtumikia Mungu(WAGALATIA 5:7-12).
Kama unapenda kuishi maisha yanayompendeza Mungu ni lazima kuudhiwa(2 TIMOTHEO 3:12).
Vyombo vya kabatini(watu wasiotumika) haviwezi kuhimili mikikimikiki matokeo yake ni kuvunjika(kuzimia/kufa kiroho).
Mpishi(Mungu) hupenda sufuria(mtu) ambalo huharakisha kupika(kutenda kazi), yaani fasta fasta na sufuria(mtu) hilo mpishi(Mungu) akilikosa huumia. Watu kama hao katika kanisa wanapopatwa na matatizo, kanisa huumia juu yao.
Fanya kazi ya Mungu ili Mungu akusafishe.
Usifanye kazi ya Mungu kwa kumtegea Fulani yamkini huyo hajapatiwa Ufunuo juu ya hiyo kazi.
Unapopata Ufunuo wa kufanya kazi ya Mungu iwe ni kuomba, kutoa n.k usisubiri mtu mwingine, huyo ni Ufunuo Kwako na si kwa mwingine.
Fanya kazi ya Mungu wewe kama wewe kutokana na Ufunuo ambao Mungu amekupatia.
Kila mtu HUSAFISHWA(hubarikiwa na kuinuliwa) kutokana na jinsi anavyotumika kama Mungu alivyompatia maoni/ mafunuo.
Tunaomba wala hatujibiwi kwa sababu hatutaki kutumika.
Mtu ambaye hatumiki huwa amejaa kinyongo, wivu, chuki, maaengenyo na kila aina ya dhambi, mtu huyo anapotumika Mungu humuosha na kuwa safi. Usipende kujaza mabaya moyoni kwa kufanya hivyo utakufa wakati siku siyo zako. Bwana akutoe huko katika Jina la Bwana! Sema Amen. Lazima vitu vingine tuvishinde na tuvitupe nje katika Jina la Bwana.
Tunaweza kushinda baada ya Mungu kutuosha na kuwa huru mbali na dhambi kwa kumaanisha kuziacha ( 1 YOHANA 1:5).
Tuyafanye mapenzi ya Mungu ili tuzidi kuwa safi. Ili kuzidi kuoshwa ni lazima uzaliwe mara ya pili yaani uokoke (MATENDO 20:28-31)na ni lazima tununuliwe kwa Adamu ya Yesu ili tuzidi kuwa safi. Tukioshwa kwa damu ya Yesu ndipo tunapokuwa na Sifa ya kuwa vyombo vya kutumika vinavyomfaa Bwana kwa kazi njema. Tunakombolewa kwa damu ya thamani (1 PETRO 1:16-25).
Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote yule hata kama yeye(mtu huyo) anajiona hawezi .Isaya alikuwa tayari kutumika, tatizo midomo yake ilikuwa ni michafu akamwomba Mungu amsafishe ndipo akawa safi na kuanza kutenda kazi ya Mungu kwa viwango vya juu sana(ISAYA 6:5-7).
Kama unataka Mungu akutumie kwa viwango vya juu, jambo la kwanza ni kuwa muwazi kwa Mungu, kumwambia tatizo alilonalo aliondoe kisha mwambie akufanye chombo chake kimfaacho kwa kazi njema. Mungu anaweza kutusafisha, cha msingi ni sisi kuwa tayari na kumwambia Mungu tuko hapa kama Isaya (ISAYA 6:8).
Jihoji mwenyewe, Je! Wewe ni chombo gani kwake Mungu? Je! Mungu ana kuthamini? Una thamani gani katika nyumba ya Mungu? Kama huna thamani mbele zake mwombe Mungu akufanye uwe chombo cha jikoni, jikoni ndikokunakotoka kila kitu, tusikubali kuwa vyombo vya kabatini.
Written by Zachary John Bequeker - Mwanza Tanzania. +255625966236.
Kwa Masomo zaidi tembelea www.zakachekainjili.blogspot.com
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: