» » SOMO: BAADA YA KUOKOKA TUKO HURU MBALI NA DHAMBI



»Mtu huwa mtumwa wa kile anachokitii(kukitumikia) ,kama anatii dhambi, basi dhambi humtawala kwa sababu hiyo atafanya mambo yamchukizayo Mungu kwa maana hiyo atakuwa mtumwa wa dhambi aliye mbali  na haki (WARUMI 6:20).

 »Kama anatii katika haki, yaani Neno la Mungu, anakuwa mtumwa wa haki na anakuwa yuko mbali na dhambi yaani matendo ya giza(WARUMI 6:18,22).

»Kabla ya mtu kuokoka anakuwa yuko chini  ya dhambi, anapookoka anakuwa huru, si huru kufanya lolote bali anakuwa huru na kuhesabiwa haki mbali na dhambi(WARUMI 6:11).

»Mtu aliyeokoka ni mtumwa wa haki, maana yake anapaswa kuyatenda yale yote yampendezaye Mungu; Unapowekwa huru mbali na dhambi unakuwa mtumwa wa haki.(WARUMI 6:17-18).

»Kumbe, baada ya kuokoka si kwamba tuko huru kufanya jambo lolote lile bali kinachofanyika ni kubadili tu aina ya kazi, Ulikuwa unatumikia dhambi basi unaamua kuachana na dhambi na kumtumikia Mungu kwa kuyatenda yale yote aliyotuagiza(ZABURI 119:9).

»Pia tuvae mavazi yanayompendeza BWANA. Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamke wala mwanamme asivae mavazi yampasayo mwanamke (KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5)
»Tunapoongozwa na Roho tunakuwa hatuko chini ya sheria ya dhambi (WAGALATIA 5:18).

»Tunapaswa tuwe wafu katika dhambi. Mtu aliye kufa hawezi kufanya lolote, hivyo nasi tunapoifia dhambi tunakuwa hatuwezi tena kutenda yale yamchukizayo Mungu (WARUMI 6:11).

»Baada ya kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha, tunakuwa tumeacha(resign) kufanya kazi za shetani na Kuanza kufanya kazi za Mungu ambazo matendo mema yampendezayo Baba yetu wa Mbinguni.

»Kama umeokoka na unasema kuwa uko huru kufanya chochote, ndugu yangu umepotea...hebu badilika sasa.

»Ikimbie Misri(dhambi) sasa yaani utumwa wa Farao(Shetani) ufanywe mtumwa wa Mungu ambapo kuna kutakaswa na matokeo yake ni uzima wa milele(WARUMI 6:22).

»Pasipo utakatifu hatuwezi kumwona Mungu.

»Kama bado hujaokoka, huu ni muda wako sasa.
 Fuatisha sala hii. Sema
" Bwana Yesu, mimi ni mwenye dhambi, shetani amekuwa akinitumikisha katika dhambi, lakini sasa naamua kwa dhati ya Moyo wangu kuacha kazi zake na kuingia katika kazi yako ili nitendeyale yote yakupendezayo wewe. BWANA Yesu, futa Jina langu katika vitabu vya hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima wa milele katika Jina la Yesu..Amen"
Sasa umeokoka, tafuta kanisa linalohubiri wokovu kwa msaada zaidi.
Kwa msaada wa kiroho, ushauri, maombi wasiliana nasi kwa WhatsApp/SMS +255-625-966-236.
Ni mimi Ev. Zachary John Bequeker- Mwanza Tanzania.
            
                    <= CHANGIA HUDUMA HII=>

Mungu akubariki sana!!!

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply