»Jeshi lililogawanyika haliwezi kushinda hata kama lina zana/silaha nyingi za kivita. Kinachofanya Jeshi kushinda ni UMOJA.
»Kipindi cha vita ya Idd Amin na Tanganyika, Upande wa Jeshi la Idd Amin walikuwa na silaha nzitonzito za kivita kiasi kwamba hata wanajeshi wa Tanganyika walipokuwa wakizifanya mateka ililazimika baadhi ya wanajeshi wa Uganda wawaelekeze namna ya kuzitumia silaha hizo. Pamoja na Idd Amin kuwa na silaha nyingi hakuweza kushinda kwa sababu Jeshi lake (Jeshi la Uganda) nilikuwa limegawanyika katika makundi mawili, moja lilimuunga mkono Idd Amin na lingine lilikuwa kinyume naye. Tanganyika ilifanikiwa kumpiga Idd Amin kwa sababu ya UMOJA.
»Watu waliookoka ni askari katika Jeshi la Kristo.
»Mungu ni Bwana wa Majeshi (1 SAMWELI 17:45, ZABURI 46:7, ISAYA 1:24)
»Paulo na Watakatifu wenzie walikuwa ni Askari katika Jeshi la Bwana (WAFILIPI 2:25, FILIMONI 1:1-3).
»Tunapaswa tuwe askari wema wa Kristo Yesu(2 TIMOTHEO 2:3).
Askari hunia mamoja, hufanya kazi kwa pamoja kwa kujua kuwa ushindi huja kwa sababu ya UMOJA.
»Tufanye kazi ya Mungu kama askari, tuzungumze kama askari wa Yesu.
»Askari hana mambo ya hekima, akisikia mguu pande ni mguu pande hakuna cha kuanza kujifikiriafikiria na kusema"hivi huyu hajui nimechoka? hatumii hata hekima! kwanza mimi namzidi umri" bali ni kutii mara moja. Na sisi tutii maagizo ya Mungu mara moja bila kufikirifikiri.
» Yesu na Baba ni wamoja hivyo nasisi lazima tunie mamoja na hakika tutaona tukishinda (YOHANA 17:11,20-23).
=> Jeshi lenye umoja hupanga mipango ya kivita pamoja na hufanya mashambulizi pamoja.
=> Mungu hulitumia Jeshi lenye umoja akilipatia maarifa namna ya kupambana na adui zao.
» Miaka kadhaa iliyopita Misri ilikuwa imepanga kuishambulia Israeli lakini kwa sababu ya umoja wa Jeshi la Israeli lilipanga mipango yake kijeshijeshi namna ya kuwadhibiti maadui zao kabla hawajawashambulia. Wakiwa bado uwanja wa ndege(Misri) wanajiandaa kwenda kushambulia,Israeli ilituma mashambulizi chini kwa chini na kushambulia pale pale uwanjani.
»Nasi tunapokuwa na umoja tutapita chinichini kutafuta maadui zetu wa kiroho wako wapi na kuwashambulia.
»Jeshi lililogawanyika lina wazinzi, waasherati,waongo, wachonganishi,wafarakanishi n.k
»Kama unahitaji kukuona ushindi katika mambo yako ni lazima uhifadhi umoja.
»Kama tunahitaji kuona ushindi katika kazi ya Mungu ni lazima tuhifadhi umoja na si kuwa watu wa kuubomoa umoja(WAEFESO 4:1-6,11-16)
Preached by Bishop Nathan Meshack
Preached by Bishop Nathan Meshack
Written by EV. ZACHARY JOHN BEQUEKER - MWANZA TANZANIA +255625966236
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: