Ndoa za mitala hufanyika kwa wingi Afrika na kwa watu wa Imani ya kiislamu.
Ndoa hizi mwanamume mmoja anaoa zaidi ya mwanamke mmoja.
»Watu wengi wamekuwa wakifikiri ndoa za mitala ni sahihi na zinakubalika mbele za Mungu. Je, ni kweli? Hapana! Ili jambo liwe sahihi ni lazima liwe limekubaliwa na Mungu.
»Mungu ndiye aliyeanzisha ndoa ulimwenguni.
»Alimfanya mtu wa kwanza Adamu(MWANZO 1:26). Akaona si vyema awe peke yake. Hivyo akamfanya "MKE " kwa ajili ya Adamu.
»Kama Mungu alitaka Adamu awe na wake wengi; angemfanyia zaidi ya mmoja. Lakini aliona mmoja anatosha.
»Mwanadamu katika tamaduni zake tofauti akaleta mawazo mengi juu ya ndoa ulimwenguni. Baadhi ya mawazo ya mwanadamu huwa sawa na mpango wa Mungu. Baadhi ya mawazo ya mwanadamu hayakubaliani na mpango wa Mungu.
»Ndoa ya mitala imeanzishwa na mwanadamu (ni man-made) na si mpango wa Mungu katika ndoa.
»Chochote kile ambacho hakikubaliani au hakiendani na kile alichokifanya Mungu au kukisema ni DHAMBI.
»Mpango wa Mungu niMUME MMOJA na MKE MMOJA(MWANZO 2:21-24)
MIFANO YA WANAUME WALIOOA WAKE WENGI KWENYE BIBLIA
»Kuna mifano mingi ya mitala katika biblia.
1: LAMEKI alikuwa ni mtu wa kwanza na mwanzilishi wa ndoa za mitala. Lameki alikuwa na wake wawili. Alikuwa muuaji na hakuna jema linalotajwa juu yake(kuhusu yeye).. (MWANZO 4:19-24).
2:ABRAMU pia alikuwa katika mitala. Mke wake Sarai, hakuweza kupata watoto. Akampatia ABRAMU kijakazi wake ili azae naye. Baadaye Sarai akamwonea wivu hajiri. Ndoa hii ilikuwa imejaa shida.
3: ESAU alioa wanawake wawili wa Kihiti walisababisha huzuni kubwa kwa wazazi wake,Isaka na Rebeka. Ndoa za mitala huathiri mahusiano(MWANZO 26:34-35).
4: Gideoni alikuwa ni kiongozi Mkuu na jasiri. Alipata watoto 70 Kutoka kwa wanawake wengi. Pia alikuwa na suria(mchepuko) mmoja aliyemzalia mwana. Ni aina gani ya baba atakayekuwa mwenye watoto 70? Je, atawalea ipasavyo? Si jinsi Mungu atakavyo sisi tuwe (WAAMUZI 8:30-31).
5: Mfalme Sulemani alikuwa na wanawake 700, binti za wafalme na masuria 300(michepuko 300) . Kilichoyumbisha na kuangusha utawala wake Sulemani ni ndoa za mitala (1 WAFALME 11:3-13).
»HAKUNA popote katika biblia panapoongelea mema juu ya ndoa za mitala. Pote palipokuwa na mitala kulikuwa kumejaa matatizo, na hii haibadiliki hadi Leo. Leo ndoa nyingi za mitala zimejaa matatizo.
KANUNI ZA KIBIBLIA KUHUSU NDOA ZA MITALA
»Hebu tuone kanuni za kibiblia zinazotufundisha kinyume na mitala:-
1: Tukisoma katika MWANZO 2:23-24 "Mwanamume atamuacha baba yake na mama yake naye ataambatana(ataungana) na na mkewe" Mungu hakusema "WAKE" bali alisema "MKE".
2: Paulo analinganisha Mke na mume kama Yesu na Kanisa (WAEFESO 5:23). Kanisa ni mwili wa Kristo(WAEFESO 5:22-23). Kuna mwili mmoja tu, ambao ndio kanisa (WAEFESO 4:4) .Mwanamume angeweza kuwa na wanawake wengi kama Yesu angekuwa na makanisa mengi. Kristo ana kanisa moja pekee, hivyo mwanamume anapaswa kuwa na Mke mmoja pekee.
4: Sasa yuko tayari KUBATIZWA. Kubatizwa ni kuzikwa katika maji(WARUMI 6:3-4). Na hivi ndivyo kila mmoja anapaswa kufanya ili kuwa MKRISTO.