» » SOMO: NGUZO TATU ZA UKRISTO

By Ev Zachary John Bequeker



 »Nguzo tatu za Ukristo ni IMANI, TUMAINI na UPENDO (1 WAKORINTHO 13:13).

       1.IMANI
»Maisha  ya Mkristo ni maisha ya Imani.  Imani ni matarajio ( WAWBRANIA 11:1). Pasipo Imani, haiwezekani kumpendeza Mungu (WAEBRANIA 11:6). Imani hufanya mambo yasiyowezekana , kuwezekana(MARKO 9:23).

»Tunaokolewa kwa njia ya Imani (WAEFESO 2:8-9, WAGALATIA 2:16). Tunatakaswa kwa Imani (MATENDO 26:18).

Tunapokea nguvu ya Roho Mtakatifu kwa Imani( WAGALATIA 3:14). Tunapokea uponyaji Kutoka kwa Mungu kwa Imani (MATHAYO 9:22,27-29).

»Mungu hapendezwi na mtu asiye na Imani ( WAEBRANIA 10:38).

2. TUMAINI
»Tumaini hufanya mambo kuwa na mwanga na Furaha. Mkristo hana budi kuwa na Tumaini juu ya kuja  kwake Bwana(TITO 2:13) Asipokuwa na Tumaini hawezi kuendelea kuishi maisha yanayompendeza Mungu na hatimaye Bwana anakuja kuchukua kanisa lake anamkuta mtu huyo ameshakata tamaa. Mkristo akiwa na Tumaini hili anajiweka tayari wakati wote ( LUKA 12:36-40).

 »Kama Mkristo lazima kuwa na Tumaini, vinginevyo ni sawa na kazi bure.

»Upendo hufanya mambo yote yapendeze.

3. UPENDO
»Mungu ni pendo, hivyo asiyependa hamjui Mungu (1 YOHANA 4:8).

» Mkristo aliyejaa Upendo atazishika amri za Mungu( YOHANA 14:22-24).

»Mkristo atawapenda majirani zake, na kwa kufanya hivyo hawezi kuwafanyia mabaya kama vile kuua, kuiba mali zao, huwezi kudanganya, huwezi kuzini na mkewe/mmewe, huwezi kuwasengenya, huwezi kufurahia kuona wao wakiharibikiwa n.k(WARUMI 13:8-10).

»Nguzo kuu katika nguzo hizi tatu ni UPENDO. (1 WAKORINTHO 13:1-3).

»Hebu jihoji wewe mwenyewe,
Ndugu katika Bwana (Kanisa) tunapendana? Tunawapenda JIRANI zetu kama tunavyojipenda? Hata katika maisha yetu ya kifamilia, tunawapenda ndugu wa Mme/Mke? Tunawapenda wazazi/watoto wetu?

»Bila shaka utakuwa na majibu ya maswali hayo. Mungu akusaidie kuelewa zaidi katika Jina la Yesu.

»Uwe na juma lililojaa nguvu za kiroho katika Jina la Yesu Amen.

MAOMBI: Kila msomaji wa ujumbe huu, pokea ongezeko la Imani, Tumaini na uwe na Upendo wa Kimungu katika Jina la Yesu kristo......Amen!!!!

Ni mimi Ev. Zachary John Bequeker - Mwanza Tanzania. +255625966236/+25575859048
Wasiliana nami Facebook kwa Jina hilo.( Zachary John Bequeker).
# KWA MASOMO ZAIDI TEMBELEA BLOG HII www.zakachekainjili.blogspot.com

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply