Mpendwa msomaji, napenda kukusalimu kwa Jina la Bwana Yesu. Sema "AMEN" vyema kabisa kwa kusema Amen.
Leo Tutajifunza kwa habari ya ukahaba . Maana yake, Namna unavyofanyika , Mavazi wanayo vaa na madhara yake pia.Ni mimi Ev. Zachary John Bequeker- Mwanza Tanzania.
Bila kupoteza muda twende moja kwa moja katika somo letu.
UKAHABA NI NINI?
Ukahaba ni tendo la kufanya ngono nje ya ndoa au uhusiano unaokubalika katika jamii, tena na watu mbalimbali na kwa malipo. Watendaji wanaopokea malipo huitwa kahaba au malaya; washiriki wanaotoa malipo huitwa wateja. Kama ukahaba unaendeshwa katika nyumba maalumu mahali hapo panaitwa danguro.
KAHABA NI NANI?
Kahaba ni mtu anayejihusisha na tendo la ndoa na watu mbalimbali .
NAMNA UKAHABA UNAVYOFANYIKA NA AINA ZA UKAHABA
>Kimsingi kuna aina mbili za ukahaba.
KUSHIKAMANA NA MAKAHABA CHANZO CHA UMASKINI part 01
1. Malaya anajifanyia kazi na kuamua mwenyewe namna gani. Huyu atapatikana mara nyingi akitembea barabarani, kusubiri kwenye mabaa au kwa kutangaza namba ya simu. Wanajitangaza pia kupitia intaneti na kukutana na wateja mahali mbalimbali.
2. Malaya wanafanya kazi chini ya usimamizi wa mtu mwingine au watu wengine. Hali yao inaweza kufanana na aina ya ajira wakilipwa kwa kila tendo la ngono kutoka msimamizi anayepokea fedha; au wanatakiwa kutoa malipo kwake kutokana na mapato yao. Kundi hili lapatikana mara nyingi katika danguro, lakini wako pia barabarani katika maeneo maalumu wanapotazamiwa na kuwadi. Katika kundi hili kuna hasa aina ya utumwa wa kingono ambako mabinti na wanawake wanalazimishwa kujiuza kwa wateja. Mwaka 2009 Umoja wa Mataifa ulikadiria kwamba 79% za watu wanaouzwa ni kwa ajili ya biashara ya ukahaba ambayo imekuwa hivyo biashara ya watumwa kubwa kuliko zote za historia ya binadamu. Kila mwaka watu 800,000 hivi wanavushwa mipaka ya nchi zao kwa ajili hiyo, wakiwemo hasa wanawake, wale wenye umri chini ya miaka 18 wakiwa hadi 50%.
MAVAZI YA KIKAHABA
Hawa wote huwa wanavalia mavazi maalumu yenye lengo la kuwashawishi watu kufanya ukahaba naye.
Tusome katika kitabu cha MITHALI 7:10 " Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba.....'
Kumbe tunaona kuna mavazi maalumu kwa ajili ya makahaba ambayo watu waliookoka na wenye kumcha Mungu hawapaswi kabisa kuyavaa.
Mavazi hayo ni kama nguo zinazobana makalio, nguo zinazoonyesha maungo ya ndani kama mapaja, matiti na kiuno, suruali kwa wanawake n.k.
MADHARA YA UKAHABA
Si siri kwamba ukahaba unachangia sana uenezi wa maradhi ya zinaa, ukiwemo UKIMWI.
Mbali na hivyo Mungu anachukizwa sana na Ukahaba , na Ukahaba ni dhambi .
Na wote wenye dhambi hawawezi kuurithi ufalme wa Mungu ,mahali pao ni katika ziwa la moto ambao ni moto wa milele,. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.
WARUMI 6:23 "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Achana na ukahaba , njoo kwa YESU atakuondolea kiu ya Ukahaba.
Jambo la kufanya ni kuyakabidhi maisha yako kwa Yesu na yeye atakusamehe na kuondoa kabisa kiu ya ukahaba tena.
UKO TAYARI KUONDOLEWA KIU YA UKAHABA?
Naamini uko tayari. Fuatisha maneno haya kwa dhati ya moyo wako na baada tu ya kumaliza uataona badiliko katika masha yako.
SEMA " Mungu Baba, Mimi ni mchafu mbele zako, Nimekutenda dhambi kwa namna ya kutisha, Lakini sasa naja mbele zako nikihitaji msamaha. Nakuomba Bwana ufute jina langu katika vitabu vya hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima wa milele. Mungu ondoa kiu ya ukahaba ndani yangu kuanzia sasa niwe mtoto wako Katika jina la YESU AMEN!"
Sasa umeokoka , hamu ya ukahaba haipo tena.
Tafuta mahali penye kanisa linalohubiri wokovu kwa msaada zaidi na Mungu akubariki.
WASILIANA NAMI KWA 0625 966 236/ 0758 590 489
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: